Rais Jakaya Kikwete amewataka watanzania kumnyanyapaa mwanasiasa yeyote muovu au anaefanana na uovu, anaeyataka madaraka kwa gharama yoyote kwani mtu huyo atalipeleka taifa pabaya.

Kikwete aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 125 tangu kuingia kwa injili katika Ukanda wa Pwani ya Tanga na Milima ya Usambara, iliyofanyika katika viwanja vya Muhukenda jijini Tanga.

“Wanasiasa wanaotaka madaraka kwa njia yoyotea ile muwanyanyapae, wakatalieni kwa macho makavu, hawa si watu wema watatufikisha pabaya,” alisema rais Kikwete.

Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM aliwataka viongozi wa dini kutojiunga na makundi ya wanasiasa bali wawashauri na kuwakemea wale wanaotaka madaraka kwa kununua wananchi.
“Tuwakemee wanawanasiasa wapenda madaraka kwa gharama yoyote, ambao watataka kutumia fedha kununua ushindi au ubaguzi wa rangi, kabila, dini na kadhalika, kuwabagua wapinzani wao na kujijenga kiasisa,” alisema.

Aliwataka viongozi hao wa dini nchini kuwashauri pia waumini wao na kuwaasa kutumia haki na wajibu wao kujiandikisha, kupiga kura na kuwachagua viogozi wanaofaa kuiongoza nchi.

Kauli ya kikwete imekuja wakati zikisalia siku saba nzito za maamuzi katika Chama Chama Cha Mapinduzi ambapo majina ya watangaza nia 38 yatachujwa katika ngazi mbalimbali kabla ya kutangaza majina matano yatakayopita kuelekea hatua ya pili ya mchujo.

Hatimaye, chama hicho kitamsimamisha mgombea mmoja atakaewania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Chemical: Mimi Ndiye Rapa Bora Zaidi Wa Kike Tanzania
Rapa Wa Afrika Kusini Ampiga Shabiki Jukwaani