Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete amezungumzia uamuzi uliotangazwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kurudia uchaguzi wa Zanzibar na kueleza kuwa chama hicho kiliukubali kwa shingo upande kwani kilikuwa kinajiandaa kusherehekea ushindi.

Dk. Kikwete ameyasema hayo leo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya CCM zilizofanyika katika uwanja wa Nanfua mjini Singida.

Wahudhuriaji miaka 39 ya CCM

Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya CCM

“Tulilijadili… Tulikubali kwa shingo upande, kwa sababu sisi tulikuwa tunajiandaa kusherehekea ushindi,” alisema.

Mwenyekiti huyo wa CCM aliwaomba wanachama wa chama hicho walioko Zanzibar kujitokeza kwa wingi kushiriki katika marudio ya uchaguzi ho.

“Tunawaomba wana CCM wa Zanzibar, wajiandae kwa ukamilifu kushiriki uchaguzi huo kama ilivyoelekezwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar,” aliongeza.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli, Mako wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wote wa ngazi za juu wa CCM.

 

Tetemeko kubwa la ardhi laleta maafa, laangusha jengo la ghorofa 17
Wamiliki wa Twitter wapambana na Akaunti za Magaidi wa IS