Kufuatia kuondolewa kwa Simba SC na Young Africans katika michuano ya kimataifa ngazi ya vilabu barani Afrika, Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amewataka viongozi wa klabu hizo kongwe nchini kujitathmini.

Mbali na viongozi wa klabu za Simba SC na Young Africans, Ridhiwani pia ameoneshwa kushangazwa na mashabiki wa soka nchini kwa namna ambavyo wanazisifu timu hizo kwa kutoa suluhu ugenini na kushindwa kupata matokeo viwanja vya nyumbani.

Young Africans iliondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Township Rollers ya Botswana baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 jijini Dar es salaam na kisha jumamosi iliyopita kutoa suluhu ugenini hivyo kutupwa nje ya michuano.

Simba SC walitupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na klabu ya Al Masry ya Misri baada ya kutoa sare ya mabao 2-2 jijini Dar es salaam kabla ya jumamosi usiku kutoa suluhu na kutolewa kwa sheria ya bao la ugenini.

”Magazeti yetu na washabiki wetu wanavyozisifia timu zao kwa matokeo ya Jana unaweza sema wameshinda. UJINGA MTUPU yaani NAWASHANGAA SANA. Kwa sifa zipi hizo Suluhu za Ugenini na Kushindwa kutumia Viwanja vya Nyumbani. AIBU KWENU Viongozi wa Mpira.Jipangeni Vizuri Mashindani ni Kushinda”, ameandika.

Azam FC kujipima kabla ya kuwavaa Mtibwa Sugar
Bocco awatuliza mashabiki wa Simba