Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za pongezi kwa timu ya taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) baada ya kutinga fainali ya CECAFA 2017.

Zanzibar Heroes imetinga fainali baada ya kumfunga 2-1 bingwa mtetezi wa michuano hiyo timu ya Uganda kwenye mchezo wa nusu fainali ya CECAFA Senior Challenge uliofanyika katika uwanja wa Moi mjini Kisumu nchini Kenya.

“Nawapongeza Zanzibar Heroes kwa kututoa kimasomaso na kutinga fainali. Nawatakia kila la kheri katika mechi ya fainali waibuke na kombe na watupe raha ambayo Watanzania tumeikosa kwa muda mrefu”, ameandika Dkt. Kikwete kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Hata hivyo, Zanzibar Heroes itacheza mchezo wa fainali siku ya Jumapili dhidi ya wenyeji Kenya. Katika michuano hiyo Tanzania bara iliwakilishwa na timu ya Kilimanjaro Stars ambayo haikufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua ya makundi ikiwa na alama moja tu.

 

Hijab yazua gumzo, msichana azuiwa kwenye ‘graduation yake’
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 16, 2017