Jumla ya wafungwa 74 waliopata msamaha wa Rais, Dkt. John Magufuli waliopo mkoani Katavi wamepatiwa hekari 370 za aridhi ili ziwasaidie kwenye kilimo.

Sehemu hiyo ya Ardhi imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Juma Homera, kwa hekari 5 kila mfungwa na kuagiza wazitumie kwa shughuli za kilimo ili kujipatia kipato na kuachana na vitendo vya ukiukaji wa sheria.

Wafungwa hao 43 ni kutoka gereza la Mpanda na 31 ni kutoka gereza la Kalilankulukulu.

Akitangaza kuwapa ardhi hiyo Homera alisema “Mnatakiwa kumshukuru Rais aliyetoa msamaha huu, nami natoa hekari 5 kwa kila mfungwa ikiwa ni moja ya kuwasaidia msirudie tena kufanya makosa, mkajikite kwenye kilimo, najua mtakuta familia zenu zimesambaratika nendeni mkaanze maisha upya”

Hata hivyo maeneo ambayo watagawiwa yapo kwenye wilaya za Tanganyika na Nsimbo ambayo Serikali ya mkoa wa Katavi inaendelea kuwagawia wananchi.

Video: Magufuli atangaza Ndege iliyokamatwa Canada yaachiwa
Wanaume wenye michepuko hatarini kupata tezi dume