Inakadiriwa kuwa wanawake 50 na 70 nchini Uingereza hushambuliwa kwa tindikali kila mwaka, na Shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake nchini humo huwadumia walionusurika na mashambulio hayo

Mwaka 2016, ripoti ya Serikali ilibainisha kuwa zaidi ya theluthi moja ya Wanawake ambao wako katika mahusiano au walikuwa kwenye uhusiano ya kimapenzi hunyanyaswa kwa njia moja au nyingine

Moja kati ya matukio ya shambulio la tindikali lilimuhusu Atsede Nguse aliyeolewa mwaka 2012, aliyepigwa hata wakitofautiana kitu kidogo. Mwaka 2015, alipigwa na mumewe hadi meno yake yakang’oka ndipo alipoondoka na kurudi kwao

Alianzisha maisha yake mwenyewe kwa biashara ya kuuza ‘perfumes’. Mwaka 2017, mumewe alimfuata binti huyo na kumshambulia kwa tindikali iliyomchoma vibaya na kumharibu, aliungua mikono, uso, kifua, masikio na mguu wake mmoja ambapo pia alipoteza uwezo wa kuona

Hakuweza kupata matibabu katika hospitali za Ethiopia na hakuwa na uwezo wa kifedha wa kutafuta matibabu mahali pengine popote.

Maambukizi ya Corona Nchini China yazidi kupungua
TFF yafumua na kuunda upya kamati zake