Leo Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli anakabidhiwa mfumo mpya wa mawasiliano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wenye mlengo wa kusimamia Mawasiliano ya Simu (TTMS).

Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James kilaba amesema kuwa mfumo huo unafaida kubwa katika nchi yetu hasa kiuchumi.

Baadhi ya faida hizo ametaja kuwa ni pamoja na uwezo wa mfumo huo kuhakiki mapato yote ya watoa huduma za mawasiliano na kugundua mawasiliano ya kughushi.

Pia mfumo huo kuwezesha upatikanaji wa takwimu za mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje ya nchi.

Mfumo huo pia utasaidia kugundua mawasiliano ya simu ya ulaghai na kutambua mapato na takwimu za miamala ya fedha mtandaoni na kusimamia kwa ufanisi ubora wa huduma za mawasiliano na kusaidia kuboresha viwango vya huduma hizo.

Aidha fuatilia hapa moja kwa moja kutoka ofisi ya TCRA makabidhiano ya mfumo huo mpya wa mawasiliano, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, John Joseph Pombe Magufuli.

Nairobi: Aliyewahudumia magaidi asimulia walivyomuacha wakimpa ujumbe
Baraza la Habari Kenya laikalia kooni New York Times, laipa saa 24