Zlatan Ibrahimovic, 34, atasaini mkataba wa mwaka mmoja Manchester United siku ya Ijumaa. Mchezaji huyo pia atapewa kitita cha pauni milioni 4 kama bakshishi ya ‘uzalendo’ kutoka PSG (Gianluca Di Marzio).

AC Milan wanakaribia kuuza hisa kiasi kubwa kwa kundi la wawekezaji kutoka China ambao wanataka kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 23 (Gazzetta dello Sport)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger atakutana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Ufaransa na Lyon, Alexandre Lacazette, 25, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 45 (Sun)

Leicester City wanazungumza na Norwich kutaka kumsajili winga Robbie Brady, 24 (Leicester Mercury)

Beki kutoka Serbia Neven Subotic, 27, aliyenunuliwa na Jurgen Klopp alipokuwa Borussia Dortmund amethibitisha kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo (Daily Express)

Chelsea watapanda dau kwa mara ya tatu kumtaka kiungo wa Roma Radja Nainggolan wiki hii na pia kiungo wa Leicester N’Golo Kante, 25 (Daily Mirror)

Southampton wanapanga kumtangaza Mfaransa Claude Puel kuwa meneja mpya wiki hii (Daily Telegraph)

Mshambuliaji wa Spain na Celta Vigo, Nolito, 29, amesema anasikia fahari kuhusishwa na Manchester City na Barcelona, lakini kwa sasa anafikiria michuano ya Euro 2016 (La Vanguardia)

Borussia Dortmund wamepanda dau kumtaka mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Karim Bellarabi, 26, kwa kuwa wanatarajia kuondoka kwa Henrikh Mkhitaryan, 27, anayedhaniwa kwenda Manchester United (Daily Mirror)

Uhamisho wa Mkhitaryan kwenda Old Trafford unakaribia kukamilika baada ya maafisa wa Dortmund kwenda Manchester kuzungumzia dau la United kwa kiungo huyo kutoka Armenia (Sun)

Paris St-Germain wanamnyatia kiungo wa Sevilla Grzegorz Krychowiak, 26, na wako tayari kulipa pauni milioni 32 (Marca)

Beki wa Barcelona Dani Alves, 33, anakaribia kuhamia Juventus na huenda akafanya vipimo vya afya siku ya Jumatatu (Goal.com).

Shukrani Kwa Salim Kikeke

Video: Taarifa kutoka Wizara ya afya kuhusu mlipuko wa ugonjwa usiofahamika Dodoma
Video: Wateule 75 wa Kikwete waliotemwa hawa hapa. Watanzania mil. 39 wanakunywa mataputapu - Magazeti leo