Mahakama Kuu ya Tanzania imeridhia kuwapa dhamana maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanaokabiriwa na kesi ya upotevu wa makontena 349 bandarini yaliyoisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu umetolewa jana kufuatia maombi ya dhamana yaliyowasilishwa mahakamani hapo na washitakiwa hao wakiongozwa na aliyekuwa Kamishina wa forodha wa Mamlaka hiyo, Tiagi Masamaki.

Aidha, Mahakama Kuu ilitoa masharti ya dhamana hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja, kuwasilisha wadhamini watakaokuwa na uwezo wa kusaini hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja pamoja na kuwasilisha hati zao kusafiria.

Vigogo hao walikamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani baada ya ziara ya kushtukiza iliyofanywa bandarini na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kubaini upotevu wa makontena yaliyopita bandarini hapo bila kulipa kodi huku uchunguzi ukibaini uhusika wao katika mchakato huo.

CCM Yajibu hoja kuwa baraza la Mawaziri linaipunja Zanzibar
Homa ya Nguruwe yaibua taharuki Mwanza, Watu wakimbia ‘Kitimoto’