Mchungaji Timothy Wanyoike mwenye umri wa miaka 40 afumaniwa akifanya mapenzi na Binti aliyetambulika kwa jina la Scholar Kariuki mwenye umri wa miaka 21.

Taarifa zinasema kuwa fumanizi hilo limefanywa na mume wa binti huyo bwana Kariuki Macharia.

Mume wa binti huyo amesema kuwa alikuwa akihisi uhusiano baina ya wawili hao kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita.

Amesema alikuwa akimchunguza mke wake kupitia simu yake ya mkononi na kuangalia jumbe ambazo mchungaji alikua akimtumia mkewe.

Baada ya kugundua mchungaji anatoka na mke wake aliwawekea mtego ili kujihakikishia juu ya mahusiano ya mkewe na mchungaji, ndipo alipoamua kumdanganya mkewe kuwa anaenda safari na atatumia siku kadhaa.

Alirudi gafla na kumfumania mke wake na mchungaji kitandani wakifanya yao, alianza kumpiga yule mchungaji kwa hasira na kusababisha ugomvi mkubwa sana.

Mpaka polisi walipokuja na kuingilia kati na kumkuta mchungaji tayari ameumizwa ameumizwa vibaya wote walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi cha Nyeri kutoa maelezo zaidi.

 

Mpina atoa mwezi mmoja kukamilishwa kwa mradi wa maji
?LIVE: Rais Dkt. Magufuli akiongea na wananchi wa Mkanyageni, Muheza Tanga