Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameagiza makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma yajengwe katika kata ya Mahembe kama ilivyopendekezwa awali na Baraza la Madiwani na si katika eneo la Kamala linalopendekezwa na watalaam hivi sasa, ambapo ameikabidhi jukumu hilo kwa TAMISEM kuhakikisha wanalisimamia.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo baada ya kusimamishwa na Wakazi wa kata hiyo akiwa njiani kwenda kukagua shamba la michikichi katika gereza la Kwitanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Kigoma.

Aidha Wakazi hao wa kata ya Mahembe wamemweleza Waziri Majaliwa kuwa wamesikitishwa na hatua ya kubadilishwa kwa mapendekezo hayo ya awali yalitolewa na Madiwani.

Waziri Mkuu ameagiza kama sababu ni eneo la kata ya Mahembe kutofaa kwa ujenzi wa majengo ya ghorofa, basi ramani ibadilishwe ili yajengwe majengo ya kawaida.

Amesema Serikali inathamini na kuheshimu uamuzi ya Wananchi ambao tayari wamejitolea ardhi yao yenye ukubwa wa hekari 25 kwa ajili ya ujenzi huo wa  makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Kigoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi wa kijiji cha Mahembe wilayani Kigoma wakati aliposimama alikiwa njiani kwenda kukagua shamba la michikichi la Gereza la Kwitanga, Septemba 17, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisikiliza swali kutoka kwa  Hussein Ali Makorokocho  (kushoto) wakati aliposikiliza  na kuzitolea maelekezo kero za wananchi katika kijiji cha Mahembe wilayani Kogoma.  Aliimama kijijini hapo akiwa njiani kwenda gereza la Kwitanga kukagua kilimo cha michikichi, Septemba 17, 2021.
Ruto asema yupo tayari kufanya suluhu
Akamatwa kwa kuchezea nyeti za mtoto