Uongozi wa lebo ya muziki ya @kondegang umetoa taarifa kwa umma kuweka wazi makubaliano ya kusitisha mikataba na Wasanii wawili waliokuwa chini ya lebo hiyo @officialkilly_tz na @officialcheed.

Uongozi wa lebo ya muzuki ya Konde Music worldwide umetoa taarifa kwa umma yenye kubainisha kuwa lebo hiyi imesitisha makubaliano ya kuendelea kufanya kazi na wasanii wawili waliokuwa wakisimamiwa na lebo hiyo Killy pamoja na Cheed

Barua hiyo iliyochapishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Konde Gang inasomeka kwa mtiririko ufuatao;

TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa Konde Music Wordwide Unachukua Fursa Hii
Kuutaarifu Umma Leo Tar 10/10/2022 Tumefikia Makubaliano Na Wasanii Tajwa Hapo Chini Ya Kusitisha Mkataba Kutokana Na Sababu Mbali Mbali
Zilizo Nje Ya Uwezo Wetu.

  1. Ally Kili Omary Aka (Killy)
  2. Rashid Daudi Mganga Aka (Cheed)

Kwa Hiyo,Wasanii Hawa Watakua Wasanii Huru Na Kuweza Kufanya Kazi Na-Kuingia Mkataba Na Kundi Au Mtu Yeyote Na Kuendeleza Kazi Zao, Kwani Tunaamini Ni Vijana Wasanii Wenye Uwezo Mkubwa Wa kufanikiwa Katika Safari Ya Muziki.

Muonekano wa Barua.

Aidha, Konde Music Worldwide Haitahusika na Jambo Lolote Litakalohusisha Wasanii Hawa Kuanzia Tarehe Tajwa Hapo Juu.

Tunapenda Kuwashukuru Killy Na Cheed Kwa Ushirikiano Wao Katika
Kipindi Chote Cha Kuwa Pamoja na Tunawatakia Mafanikio Mema
Katika Kazi Zao Hapo Baadae.”

Kikosi kazi chavuruga ngome ya Al-Shabaab kibabe
Vikwazo vya kibiashara Tanzania na Kenya kupatiwa ufumbuzi