Zaidi ya kilo 4,880 za Sukari yenye thamani ya Shilingi Milioni 13.2 zilizokuwa zinaingizwa nchini kwa magendo na kukamatwa, zimegawanywa kwenye taasisi mbalimbali Mkoani Songwe leo Januari 5, 2021. 

Mkuu wa Mkoa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amegawa sukari hiyo kwa taasisi za Magereza, Hospitali, shule na kwenye kituo cha kulelea watoto yatima.

Akizungumza wakati wa ugawaji huo Mwangela amewaonya wafanyabiashara kuacha kuingiza sukari nchini kwa magendo kwani kufanya hivyo kunaweza kuwasababishia kufilisika watakapokamatwa. 

Mkuu wa wilaya ya Momba Mkoani Songwe Jumaa Said Irando amesema sukari hiyo imebainika wakati wakifanya operesheni kukamata bidhaa ambazo haziruhusiwi kuingizwa nchini.

Australia yasema Assange yuko huru kurejea nyumbani
Shule binafsi zaonywa kupandisha ada