Siku moja baada ya mkutano mkuu wa wanachana wa klabu ya ya Simba kuridhia maamuzi ya kumsimamisha uanachama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya klabu hiyo Hamis Kilomoni, mkongwe huyo ameibuka na kujibu mapigo.

Akizungumza juu ya maamuzi hayo ya mkutano mkuu uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, mzee Kilomoni amesema msimamo wake juu ya kile alichokuwa akikitetea upo vilevile na hajaubadilisha.

Mzee Kilomoni ameongeza kuwa yeye na wenzake ndiyo waasisi wa Simba, hayo maamuzi yaliyofanywa jana hayamtishi na wala yeye hatabadili uamuzi kwa kuwa anaamini kile anachokifanya.

Amesisitiza kuwa keshi aliyofungua itaendelea vilevile lakini kama kutakuwa na sheria zimefuatwa juu ya sakata hilo basi yeye hatakuwa na kipingamizi lakini ka hali ilivyo sasa, hakuna ambacho anaona kimembadilisha.

Habari picha za Rais wa Misri alivyowasili nchini mapema hii leo
Lukuvi awatega viongozi wa halmashauri na majiji nchini