Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un ameitupia lawama Marekani kwa kuwa chanzo cha wasiwasi katika rasi ya Korea.

Vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini hii leo vimeripoti Kim Jong Un ametoa lawama hizo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho ya kijeshi akisema Marekani ndio chanzo cha kukosekana kwa ustahmilivu kwenye eneo hilo.

Kim Jong Un amesema serikali ya rais Joe Biden imekuwa ikisema haina ugomvi na Korea Kaskazini lakini ana wasiwasi mkubwa kama kuna watu ama taifa linaloamini hilo.Kiongozi huyo amesema hakukuwa na msingi wowote wa Marekani kuchukua hatua dhidi yake iwapo hakuna mvutano kati yao.

Aidha Kim ameilaumu Korea Kusini kwa undumila kuwili akisema majaribio yake hatari ya kujiimarisha kijeshi yanavuruga usawa wa kijeshi katika rasi ya Korea na kuongeza hali ya wasiwasi.

Gomes: Chama, Miquissone wameshakwenda, tuwaamini waliopo
Dkt.Gwajima kumuwakilisha Rais Samia Kongamano la Tatu la Kimataifa la Wanawake-Urusi