Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un amesema kuwa yuko tayari kukutana kwa mara ya tatu na Rais wa Marekani, Donald Trump lakini ametoa masharti.

Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya Rais Trump kueleza kuwa anatarajia kuwa kutakuwa na mkutano wa tatu kati yake na Kim.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA), Kim amesema kuwa kama Trump anataka warejee tena mezani ni lazima Marekani iachane na namna ambavyo inafanya mahesabu yake na kufikiria upya.

“Tunachotaka, Marekani iachane na mahesabu waliyonayo sasa, na waje na mahesabu mapya,” Kim anakaririwa na KCNA katika hotuba yake kwa Bunge.

Trump na Kim wameshakutana mara mbili, Juni mwaka jana nchini Singapole na Februari mwaka huu Hanoi nchini Vietnam, wakijaribu kufikia muafaka wa kuondoa taharuki kati ya nchi hizo mbili lakini walishindwa kukubaliana kuhusu masharti ya kuondoa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini ili nchi hiyo iweze kuachana na mpango wa makombora ya kinyuklia.

CAG: Kuna upungufu wa mabasi 165 ya mwendo kasi
LIVE: Rais Magufuli Akizindua Mji wa Kiserikali Ihumwa