Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un amefanya mabadiliko kwenye kiapo cha Taifa hilo ambacho humhusu kila mwananchi, akiwapunguza babu yake na baba yake.

Kwa mujibu wa ripoti, kiapo hicho kilichokuwa na kanuni 10 kimepunguzwa hadi kanuni 5 na kwamba baadhi ya yaliyoondolewa ni yale yalikuwa yanasifu mafanikio na fikra za mwanzilishi wa taifa hilo, Kim Il-sung ambaye ni babu yake, pamoja na Kim Jong-il mwana wa muasisi huyo aliyeshika madaraka mwaka 1994.

Wananchi hutakiwa kutamka kiapo hicho wakiwa wamenyoosha mkono mmoja juu kama ishara ya kuonesha utii wao kwa viongozi na uzalendo kwa nchi yao, kwa mujibu wa gazeti la DailyNK.

Rais wa Korea Kaskazini wanatakiwa kuishi kwa kufuata waliyonena ndani ya kiapo hicho wawapo nyumbani, kwenye huduma za kijamii, kwenye biashara, shuleni na hata sehemu za kazi.

Imeelezwa kuwa Kim Jong Un ameongeza vipengele ambavyo vinawafanya raia wake wawe na utii uliotukuka kwake kwake pamoja na kuwa wazalendo kwa nchi yao.

Taarifa hiyo imekuja saa chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kuwa bado kuna hatari kubwa kutoka kwa Korea Kaskazini, hivyo alirejesha vikwazo alivyokuwa amekusudia kuvitoa baada ya mkutano wao nchini Singapore.

Padri aliyempiga kofi mtoto kwenye ubatizo atumbuliwa
Rais wa Zimbabwe anusurika kuuawa kwa bomu