Mwanamitindo na muigizaji Kim Kardashian ameonekana akiendelea kushikiria msimamo wa kupigania haki za wafungwa nchini Marekani, hii ilianza pale alipotangaza kusomea sheria na hadi kufikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wafungwa kuaachiwa huru.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ Kim pamoja na mumewe Kanye West wapo njiani kumsaidia rapa Asap Rocky atoke gerezani kwa hali na mali.

Rapa huyo ambae anasubiria hukumu yake akiwa jela nchini Sweeden kwa kosa la kumpiga shabiki huenda akakabiliwa na kifungo cha miaka 6 endapo atakutwa na hatia.

Kim na Kanye wako mbioni kumsaidia rapa huyo na  imeelezwa kuwa wawili hao walikuwa kwenye mazungumzo na Ikulu ya Marekani kwaajili ya kumsaidia rapa Asap kwa kesi inayomkabili.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na kim wameuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim alifanya mazungumzo ya simu na mke wa Rais wa Marekani Jared Kushner na alimueleza kuhusu kesi ya Asap na kaifikisha ikulu kwaajili ya majadiliano.

Hata hivyo  Mwanamziki mkongwe, Snoop Dogg alitoa tamko hadharani kwa Kim na kumtaka amsaidie rapa huyo kama alivyowasaidia wafungwa wengine kutolewa gerezani na kuwa huru.

Rapa Asap Rocky alikamtwa  june 30 mwaka huu mtaa wa Stockholm Sweeden baada ya kuanzisha ugomvi na kusababisha kukosekana kwa amani eneo hilo.

Makampuni ya Ulinzi yanayo ajiri vikongwe hatarini kufutwa
Serikali kuanza kusajili nyaraka na hati miliki za ardhi ndani ya mkoa

Comments

comments