Mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian hivi karibuni amesaidia wafungwa 17 kuachiwa huru kufuatia kampeni yake ya ”90 DAYS OF FREEDOM’’ iliyozinduliwa rasmi na wanasheria wake Brittany K, Barnett ambaye anashirikiana nae katika kuendesha kampeni hiyo.

Kardashian ambaye ameungana na Barnett  pamoja na MiAngel Cody wameamua kufanya kampeni hiyo mara baada Rais wa Marekani, Donald Trump, kusaini hatua ya kwanza ya sheria inayoruhusu baadhi ya watu waliofungwa kwa tuhuma za dawa za kulevya kuomba kupunguziwa adhabu.

Kufuatia hatua hiyo kwa sasa Kim Kardashian amekuwa akipokea simu nyingi kwa watu mbalimbali wakihitaji msaada wa ndugu zao waliopo jela ili wapatiwe msaada wa kuachiwa uhuru.

Kim alianza rasmi kujihusisha na kampeni hiyo mara baada ya kumtembelea Rais, Trump Ikulu yake mwaka jana kumtetea Bi Alice Marie Johnson mwenye umri wa miaka 63 kutoka Alabama ambaye alifungwa kifungo cha maisha kwa kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya na sasa ni mmoja ya waliopokea msaada wa kuachiwa huru baada ya kutumikia kifungo jela kwa miaka 12.

Wafungwa wengine ambao Kim amewasaidia kuachiwa huru ni pamoja na Jeffrey Stringer kutoka Florida na Cyntonia Brown kutoka Tennessee ambaye ametumikia kifungo cha jela kwa miaka 12 kwa kosa la kumuua mwanaume ambaye alilipwa kushiriki nae kingono akiwa mwenye umri wa miaka 16.

Wakili Barnett amesema kuwa Kim si tu anawasaidia wafungwa hao kurudi uraiani bali anawasaidia kupata kazi na nyumba kwa ajili kuendelea na maisha.

 

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa yateketeza Nyavu na Mitumbwi Bandia
Beckham apigwa stop kuendesha gari miezi 6