Mke wa rapa Kanye West, Kim Kardashia ametumia muwakilishi wake kuzungumzia ripoti zilizosambaa kwenye mitandao zikidai kuwa ana mpango wa kuchukua video wakati anajifungua mtoto wa pili.

Taarifa hizo za awali zilizoripotiwa na mtandao wa Hollywoodlife zilieleza kuwa star huyo wa ‘Keeping Up with the Kardashians’ alikuwa na mpango wa kushuti video hiyo licha ya ukweli kuwa alifanya hata sura ya mwanae wa kwanza North West kuwa siri kubwa kwa kipindi kirefu.

Muwakilishi wa Kim Kardashian amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote. Muwakilishi huyo aliyezungumza kwa niaba ya Kim K alikanusha pia tetesi za awali kuwa Kanye West alikuwa anataka mtoto wao North West kuwa katika chumba cha kujifungulia wakati Kim atakapokuwa akimleta duniani mdogo wake.

Ray C Afanikisha Kukirudisha Kiuno Bila Mfupa
Video Mpya: Nuru The Light – L