Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limemteua Kim Poulsen raia wa Denmark kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Poulsen amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Taifa Stars ambayo hivi sasa iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta nafasi ya kucheza fainali za AFCON pamoja na kombe la Dunia ambazo zote zitafanyika 2022 katika nchi za Cameroon na Qatar.

Kocha huyo aliwahi kuinoa Taifa Stars 2012 na 2013 ambapo kabla ya kupewa nafasi hiyo alikua kocha wa timu za Taifa za vijana.

Kocha huyo anachukua nafasi ya Etienne Ndayiragije ambaye hivi karibuni alifikia makubaliano na TFF kuvunja mkataba wake.

Ndayiragije aliteuliwa kuinoa Stars mnamo Julai 2019.

Mwenyekiti wa BBI afariki dunia
Muhammed Seif Khatib afariki dunia