Ligi kuu ya soka nchini England inaendelea tena usiku huu kwa mchezo mmoja ambapo Everton watakua nyumbani Goodison Park kuwakaribisha The Egles (Crystal Palace).

Katika mchezo huo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Romelu Menama Lukaku anatarajiwa kuanza katioka kikosi cha kwanza cha Ronald Koeman, licha ya kuwepo kwa taarifa za kuugulia maumivu ya kidole gumba.

Leighton Baines bado yupo mashakani kucheza mchezo huo kufuatia maumivu ya nyonga yanayomsumbua, ili hali James McCarthy anaendelea kuwa katika hali ya kufikirikla.

Wilfried Zaha wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Crystal Palace baada ya kukosa mchezo uliopita dhidi ya Sunderland, kufuatia maumivu ya misuli ya paja.

Jonathan Benteke, ambaye ni mdogo wa mshambuliaji Christian Benteke, huenda akaendelea kuwa nje ya kikosi cha Crystal Palace baada ya taarifa za kitabibu kueleza bado anahitaji muda zaidi wa kupumzika kufuatia upasuaji wa goti aliofanyiwa.

Ligi hiyo kesho itaendelea tena kwa michezo kadhaa ambapo:

Swansea v Liverpool

Hull v Chelsea

Sunderland v West Brom

Watford v Bournemouth

West Ham v Middlesbrough

 

Picha: Serengeti Boys Wafanya Mazoezi Uwanja Wa Maamuzi
Video: Chadema yafuta Ukuta Oktoba Mosi