Serikali nchini Malawi, imetangaza hali ya hatari na maafa katika eneo la kusini mwa nchi hiyo, na kusema idadi ya watu 99 waliofariki kutokana na Kimbunga Freddy huenda ikaongezeka na kwamba Shule zitaendelea kufungwa katika wilaya 10 zilizoathirika zaidi.

Rais wa nchi hiyo, Lazarus Chakwera, amesema, ana wasiwasi mkubwa wa uharibifu ulioletwa na Kimbunga Freddy ambacho kimezipiga Wilaya nyingi katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo.

Takriban watu 99 walithibitishwa kufariki hapo jana Jumatatu Machi 13, 2023 huku Kamishna wa Masuala ya Kukabiliana na Majanga nchini humo Charles Kalemba akisema vifo vingi vilitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo Blantyre.

Awali Msemaji wa polisi wa Malawi, Peter Kalaya alisema, “Tumerekodi vifo 99 kati ya hivyo vifo 85 na watu wengine 134 waliolazwa Hospitalini ni matukio yaliyotokea jijini Blantyre pekee.”

Mashabiki Mbeya City wamlaumu Kocha Mubiru
Kapombe: Tutapambana kuimaliza Horoya AC