Kasi ya rais John Magufuli ambayo imeanza kufuatwa na viongozi wa serikali ikiwa ni pamoja na wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya imewashukia vigogo watatu wa Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mlongo amewasimamisha kazi watumishi watatu jijini humo kwa kosa la kutoa kibali cha ujenzi wa nyumba inayosadikika kuwa ni ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Pamphil Masashua.

Mlongo aliwasimamisha kazi Kaimu Meneja wa Mamlaka wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira, Nestory Kabete, Kaimu Afisa Ardhi, Richard Pingu na Mkuu wa Kitengo cha Mipango miji, Wilson James kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na uadilifu.

“Na yeyote aliyeshiriki kutoa kibali cha ujenzi na ramani ambavyo havikuwa sahihi, lazima watafikishwa mbele ya mahakama,” alisema Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza.

Mradi huo wa maji umeelezwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 20.

Magufuli Aanza Panga-Pangua Jeshi La Polisi
Mnyika Aibukia Sakata la Bandari, Asema Dawa Jipu Sio Kulitumbua