Kimbunga Fani leo kimeshambulia Pwani ya Mashariki mwa India na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali, kwa mujibu wa Idara ya Hali ya Hewa ya nchi hiyo.

Mvua kubwa imeripotiwa katika maeneo ya Orissa ambayo pia hufahamika kama Odisha, yalipitiwa moja kwa moja na kimbunga hicho.

Mji maarufu wa kitalii wa Puri pamoja na maeneo ya jirani yamekumbwa na upepo wenye kasi ya Kilometa 175 kwa saa (175km/h), kasi ambayo inatarajiwa kuongezeka hadi kilometa 200 kwa saa (200km/h).

Mafuriko yameripotiwa katika maeneo mengi na zaidi watu milioni moja wameripotiwa kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya Orissa. Watu wengine wamehamishiwa katika maeneo ya jirani kutokana na tahadhali ya kukumbwa na kimbunga hicho.

Kimbunga hicho pia kinatarajiwa kufika katika wilaya 15 za Orissa ikiwa ni mbali na Puri, eneo ambalo ni maarufu lenye masinagogi yenye umri wa hadi miaka 858.

Usafiri wa anga, maji na barabara umezuiwaliwa, shule zote za serikali na binafsi zimefungwa. Imeripotiwa kuwa bandari tatu kubwa za eneo hilo pia zimefungwa.

Serikali ya nchi hiyo imechukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kutumia helikopta kadhaa kutoa misada kwenye maeneo yaliyoathirika. Kitengo cha kutoa huduma za kimatibabu pia kimewekwa ‘standby’.

Jeshi maalum la kukabiliana na majanga la nchi hiyo, NDRF limetuma vikosi kadhaa kutoa msaada kadiri unavyohitajika.

Mengi umekwenda wapi?, JPM ampa Lukuvi maagizo mazito
Mwanamke aliyefungwa kwa kumuua kaka yake Kim Jong Un aachiwa huru