Timu ya Kagera Sugar inaendelea kufanya vibaya kwenye michezo yake ya Ligi Kuu ya Vodacom, mambo si mambo katika kikosi hicho chenye maskani yake mkoani Kagera.

Kutokana na mwenendo huo, sasa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime ameamua kutoa kauli kwa kuweka wazi juu ya msimamo wake baada ya hali ya hewa kuwa mbaya kikosini hapo.

Maxime ambaye anajulikana kuwa ni kocha mwenye maneno mengi amesema kuwa hana mpango wa kujiuzulu nafasi yake aliyonayo sasa kwa kuwa yeye ni kama baba ambaye hawezi kukimbia matatizo ya familia yake.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Kagera Sugar imekuwa na kiwango kisichoridhisha, hivyo kujikuta wakipoteza pointi nyingi licha ya kuwa wana wachezaji wazoefu wa ligi hiyo akiwemo kipa Juma Kaseja.

Maxime amesema hajakata tamaa juu ya kikosi chake licha ya kuwa anaumizwa na matokeo yanayopatikana, hivyo hawezi kuikimbia familia yake badala yake anakabiliana na matatizo ili kuyamaliza kwa kuwa anajua huu ni upepo mbaya na utapita tu.

Video: Tunashirikiana vizuri na wapinzani Ubungo- DC Kisare
Haruna Niyonzima yupo India kwa matibabu

Comments

comments