Moja kati ya majimbo ambayo masikio ya wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa na wananchi wengi hivi sasa yameelekezwa ni  lililokuwa jimbo la Kigoma Kusini ambalo hivi sasa linajulikana kama jimbo la Uvinza ambalo linatetewa na David Kafulila wa NCCR-Mageuzi.

Matokeo ya ubunge katika jimbo hilo bado hayajatangazwa hadi sasa ambapo ripoti za uhakika kutoka jimboni humo zinaeleza kuwa Msimamizi wa Uchaguzi amesitisha kuendelea na zoezi la majumuisho ya kura baada ya mgombea ubunge wa CCM Bi. Hasna Mwilima kutaka kura zilizotoka vituoni kumwagwa chini na kuhesabiwa upya badala ya kutumia fomu zilizosainiwa na mawakala, ombi ambalo lilipingwa na Kafulila.

Duru za uhakika kutoka jimboni humo zinaelezwa kuwa Bi. Hasna alikataa kuendelea na zoezi la kufanya majumuisho mara baada ya kujumuisha matokeo ya kata 5 na ndipo mvutano ulipoibuka tangu jana hadi muda huu.

Kafulila anapewa nguvu na wanafuasi wake pamoja na maagizo yaliyotolewa na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kumtaka asikubali ombi la kuhesabu upya kura kwenye masanduku kwa madai kuwa yalisafirishwa chini ya mazingira yasiweza kuaminika.

Matokeo ya jimbo hilo yanasubiriwa kwa hamu kutokana na kuwepo ushindani mkali kati ya  mgombea wa NCCR-Mageuzi na mgombea wa CCM.

 

Matokeo ya Urais Zanzibar Yafutwa Rasmi
Algeria Wataja Kikosi Cha Awali