Taasisi ya Elimu Tanzania (TIA) imeeleza kuwa bado inaendelea kufanya mapitio ya vitabu kadhaa vya darasa la kwanza vilivyobainika kuwa na makosa mengi hivyo kukosa sifa ya kutumika.

Mapema mwaka jana, TIA ilitoa vitabu vilivyoitwa ‘Najifunza kuandika’, ‘Najifunza Kuhesabu’, ‘Najifunza Afya na Mazingira’ na ‘Najifunza Michezo na Sanaa’ ambavyo vyote vilibainika kuwa na makossa.

Mkurugenzi Mkuu wa TIA, Elia Kigba amesema kuwa wanaendelea kufanya mapitio na marekebisho ya vitabu hivyo kwa mujibu wa maoni ya wadau wa elimu na kwamba ndani ya kipindi cha mwezi mmoja vitakuwa tayari kwa matumizi.

Aidha alieleza kuwa makosa yaliyofanyika ni ya kawaida kwa wachapaji na kwamba sio makubwa kama yalivyokuwa kwa vitabu milioni 2.8 ambavyo serikali iliamuru viharibiwe.

“Haya ni makossa ya kawaida tu,” alisema. “Makosa hayakuwa makubwa kama yale ambayo yalipelekea Waziri wa Elimu kuagiza vitabu zaidi ya vitabu milioni 2.8 kuharibiwa,” Bosi huyo wa TIA anakaririwa na The Citizen.

Alisema kuwa vitabu hivyo vitakavyotoka vitakuwa na ubora wa hali ya juu na kwamba lengo ni kuhakikisha watoto wanapata elimu bora zaidi.

Trump akivaa tena kitengo cha ‘ujasusi’ cha Marekani
Zitto: Hali ya chakula nchini ni mbaya