Jeshil la Polisi jijini Kampala nchini Uganda linamshikilia mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye wakati Tume ya Uchaguzi ikijiandaa kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Alhamisi wiki hii.

Kwa mujibu wa BBC, jana Polisi walizingira Makao Makuu ya Chama Cha Dk. Besigye wakati anajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari saa chache baada ya kueleza kuwa uchaguzi uliofanyika haukuwa huru na haki.

Vurugu kubwa zimeripotiwa katika jiji hilo ambapo Jeshi la Polisi limefyatua mabomu ya machozi na kuwakamata wafuasi wa Dk. Besigye waliokuwa wanaranda mitaani na waliokuwa wamefika katika makao makuu ya chama hicho.

Tume ya Taifa imeonesha kuwa hadi sasa Rais Yoweri Museven anaongoza kwa matokeo yaliyopatikana.

Jeshi la Polisi lilitahadharisha wananchi kuhakikisha wanakuwa watulivu na kuahidi kupambana kikamilifu na vitendo vyovyote vya kihalifu.

 

Utapenda majibu ya Bushoke kwa shabiki aliyetaka kujua lini atafika ‘level’ za Diamond
Rungu la waziri Mkuu latua bandari ya Tanga, atoa saa 16 kuelezwa madudu yaliyogharimu Mabilioni