Mwanamke raia wa Uingereza, Sally Jones ambaye amekuwa akihusika katika kushawishi kutoa mafunzo na kuwaajiri wanajeshi wanaojiunga na kundi la kigaidi la ISIS anamwaga machozi baada ya kundi hilo kuzuia nia yake ya kutaka kurejea nchini kwake.

Jones mwenye umri wa miaka 47, anadaiwa kujiunga na ISIS mwaka 2004 alipoingia Raqqa nchini Syria na kuolewa na mwanajeshi wa kundi hilo, Junaid Hussain ambaye alifariki mwaka juzi kwa shambulio la ‘drone’.

Mke wa mwanajeshi mwingine wa ISIS ameiambia Sky News kuwa mwanamke huyo ameendelea kumwaga machozi kila siku akiomba kurejea nchini Uingereza, ombi ambalo limekataliwa na ISIS wakidai kuwa ana sifa ya kuwa mke wa mwanajeshi wake.

“Alikuwa akilia na kuomba kurejea Uingereza lakini ISIS wamemzuia kwa sababu hivi sasa anaheshima ya kuwa mke wa mwanajeshi wa kundi hilo,” alisema mwanamke huyo.

Imeelezwa kuwa mwanae mwenye umri wa miaka 12 anatumika kama mpiganaji mtoto, na anahusishwa hadi kwenye matukio ya kuwaua mateka.

Sally Jones na familia yake

Kabla ya kujiunga na kundi hilo, Jones alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa kwenye kundi la muziki wa Rock la Krunch, na pia alikuwa akiuza marashi.

Baada ya kifo cha mumewe mwaka 2015, alitweet akieleza kuwa anaamini aliuawa na “maadui wakubwa zaidi wa Mungu.” Alisisitiza kuwa hatampenda mtu mwingine zaidi ya mumewe huyo.

Mwaka 2015, Umoja wa Mataifa ulimuwekea vikwazo Jones kama wakala wa magaidi. Alikuwa akitumia mtandao wa Twitter kuhamasisha vitendo vya kigaidi na vitisho dhidi ya nchi za Magharibi.

Moja kati ya tweets zake maarufu ni pamoja na kueleza ndoto yake ya kumchinja mfungwa mmoja wa nchi za Magharibi nchini Syria pamoja na kuwakata vichwa Wakristo.

Mwanamke huyo aliwahi kutajwa kama mmoja kati ya magaidi wanaotafutwa zaidi duniani kwenye orodha ya magaidi 20 nchini Syria.

Alitumika pia na ISIS kama mkufunzi wa vita ya kigaidi dhidi ya mataifa ya Magharibi, na aliwahi kuahidi kuwa angeitafuta pepo kwa kujilipua na bomu la kujitoa mhanga.

Sasa ameanza harakati za kutaka kurejea Uingereza, lakini ISIS wamemkatalia.

?LIVE: Rais Magufuli akizindua mradi wa maji Sengerema Mwanza
Mshambuliaji Yanga atakiwa Tottenham Hotspur ya Uingereza