Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi -CCM, Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa chama hicho  kueleza mambo mazuri kwa wananchi yanayofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kinana ameyasema hayo Jijini Dodoma hii leo Machi 21, 2023, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya viongozi  wa Umoja wa Wanawake Tanzania – UWT, kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya.

Amesema, “katika maeneo yenu hakikisheni mnakisemea Chama na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia, wala msione haya kusema ili wananchi wajue na hata katika chaguzi zijazo tusipate shida.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi -CCM, Abdulrahman Kinana.

 “Chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia katika kipindi cha miaka miwili kila kata kuna alama ya maendeleo kuanzia shule, zahanati, barabara na maendeleo ya watu, tuna kila sababu ya kujisifia na kuusifia uongozi wa mwenyekiti wa chama hiki,” amesema Kinana

Awali, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda, alisema wanawake wanaridhika na kazi zinazofanywa na Serikali na kwamba katika kipindi cha miaka miwili hakuna kitu kilichosimama na ndio maana waliandaa hafla ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi nzuri.

“Sisi wanawake wa CCM hakika tumeridhishwa na uongozi wa Rais Dk.Samia na tunaahidi katika uchaguzi wa mwaka 2025 tutatoa fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu mwanamke mwenzetu,” amesema Mary Chatanda.

Migodoro ndani ya ndoa yapata tiba kamilifu
Rais US Monastir aivulia kofia Young Africans