Mabingwa wa soka nchini Ufaransa, AS Monaco wameendelea kukiongezea makali kikosi chao ili kuhakikisha kinatetea ubingwa wake msimu ujao, kwa kumsajili winga wa kulia wa FC Barcelona Jordi Mboula.

Mboula mwenye umri wa miaka 18, zao la kituo cha kuelea na kuendeleza vipaji vya soka cha FC Barcelona (La Masia), amejiunga na AS Monaco kwa mkataba wa miaka mitano utakaofikia mwisho Juni 2022.

AS Monaco imeripotiwa kuilipa Barcelona fidia ya Euro milioni 3, ili kumnasa Mboula aliyekua amegoma kusaini mkataba mpya, baada ya kushindwa kuhakikishia namba kwenye kikosi cha wakubwa.

Mboula anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na AS Monaco baada ya Youri Tielemans, Soualiho Meite, Jordy Gaspar pamoja na Diego Benaglio.

Mwezi Februari mwaka huu Mboula aligonga vichwa vya habari vya michezo barani Ulaya baada ya kuifungia FC Barcelona bao maridadi kwenye mchezo wa michuano ya klabu bingwa Ulaya ya vijana dhidi ya Borussia Dortmund.

Kabla ya kufunga bao hilo la juhudi binafsi Mboula aliwalamba chenga mabeki wote wa Borussia Dortmund. Bao hilo lilifanya aanze kufananishwa na staa mwenzake wa Barcelona,Lionel Messi.

Taifa Stars Yaenda Afrika Kusini
Video: Ndege ya Marekani, NATO yainyemelea ndege iliyombeba Waziri wa Urusi