Mshauri wa benchi la ufundi la Taifa Stars ambaye pia ni Kocha wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni, ametangaza kuwa amepanga kustaafu kufundisha soka hivi karibuni.
Kibadeni ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa ndani ya Simba, Majimaji pamoja na Taifa Stars, amesema kwa sasa hataki presha ya timu, hivyo anataka apumzishe akili yake.
Kibadeni amesema kama mchango ametoa wa kutosha katika timu mbalimbali hivyo sasa ni muda wake wa kupumzika.
“Sitaki tena kupigishana makelele na watu wazima, unajua hizi timu zina presha sana na ukiangalia umri umeenda nimeona ni bora nipumzike.
“Hivi karibuni nitatangaza kuachana na ukocha wa hizi timu za wakubwa nitadili na kituo changu tu cha Kibadeni Sports Academy (Kisa), najua huku hawa watoto pamoja na timu kuwa siyo ya ushindani sitapata presha,” alisema Kibadeni.
Kocha huyo aliwahi kuifikisha Simba katika fainali ya Kombe la Caf mwaka 1993, lakini ikapoteza mechi ya pili kwa kufungwa mabao 2-0 na Stella Abidjan.
Rekodi hiyo inamfanya kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kwa wale wa ukanda wa Afrika Mashariki.
Chanzo: Saleh jembe
Stewart Hall Alalamikia Hujuma Ligi Kuu
CUF watoa msimamo wao rasmi na watakavyoishi na Serikali ya Dk. Shein