Msanii wa bongo fleva ambaye hivi karibuni amekuwa baba wa mtoto wa kike, na anayetamba na wimbo unaoenda kwa jina la ‘Anameremeta’ Naftal Mlawa maarufu kama Nuhu Mziwanda, tayari ameweka wazi kuhusu kusainishwa chini ya lebo ya Rockstar4000.

Nuhu ameamua kufuata nyayo za wasanii wengine kama Lady jaydee, Ommy Dimpoz pamoja na Baraka the Prince ambao tayari wameshasainishwa na wanafanya kazi chini ya lebo hiyo Alikiba akiwa Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni inayohusika na kusimamia vipindi na kazi za mastaa wa muziki Afrika.

Nuh amesema kuwa, haitakuwa busara kila kitu kikuwekwa wazi kabla ya makubaliano ya kusaini lakini mashabiki wakae wajue yupo njiani kujiunga na lebo hiyo.

“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo na lebo ya Rockstar4000 ambayo yupo Kiba na soon nitasaini mkataba. Nimekubali kufanya hivyo kwa sababu Kiba ni mtu wangu wa karibu na ninamheshimu kama kaka yangu, naamini tutafanya kazi vizuri tukiwa pamoja huko na hakuna nitakacho-pungukiwa kwa kuminywa kivyovyote vile,” amesema Nuh.

 

 

 

Mpina apiga marufuku uchimbaji na uchotaji mchanga jijini Dar
Juventus FC Yamkodolea Emre Can

Comments

comments