Mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru amewaomba marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa kumshauri Rais John Magufuli kuwakutanisha Chadema na Serikali ili kuzungumza namna ya kufikia muafaka na kuzuia kwa amani kufanyika kwa maandamano ya Septemba 1.

Chadema wamekuwa wakisisitiza kuwa watafanya maandamano nchi nzima Septemba 1 kutekeleza oparesheni waliyoipa jina la UKUTA ingawa upande wa Serikali umewatahadharisha kuwa wakijaribu kufanya hivyo ‘watakiona’.

Mzee Kingunge ambaye alikuwa kimya tangu kumalizika kwa uchauguzi wa Oktoba 25 mwaka huu, ameshauri kuwa mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye pia washiriki katika jopo la kusaka suluhu ili kusaidia uzoefu kuhakikisha nchi haiingii kwenye vurugu ya aina yoyote.

Amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kutambua kuwa hawapaswi kukaa kimya wakati huu ambapo kuna hali ya sintofahamu inayoendelea nchini.

Kingunge aliihama CCM kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kumpigia debe Edward Lowassa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema aliyeungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda UKAWA.

 

 

Video: Makonda atoa pole Jeshi la Polisi, Autaja mkakati huu kwa Wakazi wa dar
Muziki: Higher Live Version - Nikki wa Pili, produced by Dj D-Ommy