Waziri wa Maliasili na Utalii, DK Hamisi Kigwangalla amefunguka na kusema kuwa mabinti warembo na vijana wenye muonekano mzuri wanaweza kutumika katika kazi za ukarimu na kusaidia kuleta sifa nzuri za wema na uungwana kwa wageni wanaotembelea Tanzania.

Kigwangalla amesema kwa sasa wamekusudia kufanya mabadiliko makubwa katika sekta zote za huduma kwa wateja ili waweze kuwapa uzoefu wa kukumbukwa wageni mbalimbali wanaokuja nchini pamoja na kutangaza utamaduni wa nchi yetu.

”Ukarimu ni utamaduni wetu. Tunahitaji kuutumia kibiashara. Lazima tubadilike, turejeshe kwa nguvu kubwa kwenye sekta zote za huduma kwa wateja na tuutumie kuwapa wageni wetu ‘experiences’ (uzoefu) nzuri za kukumbuka waende wakatusemee kwa wenzao huko kwao, wakawe mabalozi wetu. Tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye eneo hili”.

Waziri ameendelea kusisitiza kuwa ”Tanzania tunawasichana warembo, kwa nini wasiajiriwe kwenye nafasi za kazi za ukarimu, tabasamu zao zikawa taswira ya wema na uungwana wetu kama taifa! tuna vijana imara, watanashati wanaoweza kuwa taswira ya wema na uungwana wetu, amesema Kingwangalla.

JPM apiga marufuku michango shuleni
Video: Majaliwa amkabidhi mhandisi wa maji Rorya kwa Naibu Waziri, 'hatuwezi kuwa na mtumishi wa aina hii'

Comments

comments