Kocha mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema hali ya hewa nzito ilichangia kufungwa mabao 2-0 na wenyeji African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hapo jana.

“Hatukuwa na hali nzuri kimchezo, hali nzito ya hewa imetuathiri sana, tumecheza kukiwa na kiwango kikubwa cha joto, hata hivyo ndivyo matokeo ya soka yalivyo tulichokitarajia  hakikuwa, tunakwenda Songea kwa mchezo mwingine, imani yangu  tunaweza kupata ushindi huko” alisema.

Katika mchezo wa jana, dakika 45 za kipindi cha  kwanza zilimalizika kwa timu hizo zikiwa hazijafungana,licha ya kuwepo kwa mashambulizi kadhaa pande zote mbili ikiwemo lile la  dakika ya 15 lililofanywa na Abdalah Juma  wa City  aliyefanikiwa kuwatoka mabeki wa Sports, lakini shuti lake  likashindwa kulenga lango.

Kipindi cha pili kilikuwa  kizuri kwa Sports  kwani walipanga mashambulizi vizuri na kufanikiwa kulifikia lango la City mara kadhaa ikiwemo dakika  60  ambapo  Omary Ibrahim alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la kuongoza kwa mpira mzuri wa adhabu kufuati yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la City.

Mpira ukiwa unaelekea  ukingoni Ibrahim tena  alifanikiwa kufunga bao la pili kwa  Sports  baada ya kuuwahi mpira aliotanguliziwa na Salum Isihaka na kufanikiwa kuwatoka walinzi wa City kisha  kufunga  akiwa pembeni kidogo mwa lango.

Real Madrid Na Ndoto Za Kumsajili Eden Hazard Kwa Mtego
Ratiba Ya Nusu Fainali Ya FA Kupangwa Leo