Klabu ya Mbeya City FC, imethibitisha kukamlizana na mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa ambaye alikua anacheza soka falme za kiarabu.

Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten, amezungumza na Dar24 na kueleza kuwa mshambuliaji huyo tayari ameshawasili jijini Mbeya tangu jana na uongozi ulizungumza naye.

Dismas amesema mshambuliaji huyo ameonyesha kuwa tayari kuitumikia Mbeya City na ndio maama imekuwa rahisi kwa uongozi wa juu kukaa nae chini na kuzungumza naye masuala la maslahi yake binafsi.

“Tangu jana taarifa za Mrisho zimethibitisha katika tovuti ya klabu, na amekua hapa kwa siku nzima ya leo hivyo nikuambie tu, mambo yamekwenda vyema.” Alisema Dismas

Katika hatua nyingine Dismas Ten amesema kocha mkuu Kinnah Phiri leo usiku atatangaza orodha ya wachezaji atakaowasajili, ili kukamilisha mipango yake ya dirisha dogo la usajili.

Amesema kocha huyo ameamua kufanya hivyo baada ya kuwafanyia majaribio baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao wamekuwepo mjini Mbeya kwa siku kadhaa.

“Tufanye subra, kocha atakamilisha jukumu la kutangaza orodha ya wachezaji ambao atawasajili kabla ya dirisha dogo kufungwa, ninakuomba kuwa mtulivu, maana hata mimi nina shauku ya kutaka kujua kama ilivyo kwao,” alijibu Dismas baada ya kuulizwa kuhusu usajili walioufanya.

“Kocha pia atatoa taarifa ya wachezaji walioachwa katika kipindi hiki, ima iwe wamepelekwa kwa mkopo mahala fulani ama kuondoka moja kwa moja.” Aliongeza Dismas.

Wakati huo huo kikosi cha Kagera Sugar kimewasili mjini Mbeya tayari kwa mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa mwishoni mwa juma hili katika uwanja wa Sokoine.

Kagera Sugar mapema hii leo walifanya mazoezi yao ya kwanza katika uwanja huo.

Picha: Fahamu kilicholipata jumba alilozaliwa Hitler
Mbuyu Twite Awapotezea Majimaji FC