Wajasiriamali wadogo wadogo wanufaikao na mkopo wa wanawake na vijana inayotolewa na  manispaa  ya kinondoni kupitia benki ya wananchi Dar es salaam DCB  wanatarajiwa kufanya maonyesho ya siku tatu katika viwanja vya biafra jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waaandishi wa habari afisa uhusiano  wa manispaa ya kinondoni Bw. Sebastian Mhowera  amesema maonyesho hayo yana lengo la kuhamasisha vijana na wanawake wengine kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili kujiinua kiuchumi.

DSC_0945

Aidha Bw. Mhowera ameeleza kuwa mkopo wa mfuko wa wanawake na vijana unatokana na kodi za wananchi wenyewe na hauna itikadi za kisiasa kama maneno yanavyosikika kupotosha watu.

Pamoja na hayo amefafanua mfuko huo wa kuinua wanawake na vijana ni kutekeleza agizo la serikali kuu kuzitaka halmashauri zote nchini kutenga 10% ya mapato ya ndani .

Hata hivyo pamoja na changamoto zinazokabili mifuko hiyo Bw. Mhowera amesema kwamba Manispa yake imeshkwisha weka mikakati ya kuiboresha hivyo wananchi wasisiste kujiunga katika vikundi ili kunufaika.

Mstahiki Meya wa  Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika  maonyesho hayo  ya siku tatu ya wanufaika mkopo 2729 kutoka kwenye vikundi 546 vya manispaa ya kinondoni.

 

 

Mwakyembe ataka wabunge wa upinzani wasilipwe Posho
Mbunge ataka wabakaji wanyongwe, duka la bunduki lianzishwe Zanzibar