Mwenyekiti wa mtaa wa changanyikeni, kata ya Tuangoma iliyopo wilaya ya Temeke aliyepita bila kupingwa kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka huu kwa tiketi ya CCM, Suzanne Kamugisha ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuiba milioni 12.

Imeelezwa kuwa juzi, mtoto wake aliyeajiriwa kwenye duka la simu alikutwa amesababisha hasara ya Tsh. Milioni 12 na alipohojiwa alimtaja mama yake kuwa kachukua fedha hizo kwaajili ya kampeni ya uchaguzi wa ndani ya chama.

Inadaiwa kuwa viongozi wa kata hiyo (Diwani, mtendaji wa kata na katibu kata mapema leo asubuhi walianza hatua za kuhakikisha  anatoka rumande lakini bado hawajafanikiwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Jamiiforums zinaeleza kuwa wananchi wa mtaa huo wameanza kuhamasishana kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwenye mkutano wa mtaa.

Sudan kuwalipa waathiriwa wa mabomu ya Osama, Kenya na Tanzania ya mwaka 1998
Gereza la Butimba laanza kuachia huru wafungwa