Kiongozi mpya wa kundi la Taliban nchini Afghanistan aliyemrithi Mullah Omar Mullah ametoa tamko lake la kwanza tangu achaguliwe, ambapo ametoa sharti moja litakalorejesha amani nchini humo.

Kiongozi huyo anayefahamika kwa jina la Mullah Haibatullah Akhundzada amesema kuwa ili amani irejee nchini humo, ni lazima majeshi ya Marekani na washirika wake yaondoke na yaache ushirika na Serikali ya nchi hiyo.

“Kuungana kwenu na wavamizi [Marekani] ni kama kazi ya wale walioungana na waingereza na Wasoviet katika miaka kadhaa ya historia yetu,” Akhundzada aliiambia Serikali ya Afghanistan.

Wapiganaji wa Taliban

Wapiganaji wa Taliban

Alisema kuwa uwepo wa majeshi hayo ya wageni ndani ya ardhi hiyo hakuathiri hata kidogo harakati za kundi hilo dhidi ya Serikali inayoungwa mkono na Marekani.

Haibatullah Akhundzad aliteuliwa rasmi kuwa kiongozi wa Taliban mwezi Mei mwaka huu baada ya kundi hilo kutangaza rasmi kuwa muasisi wa kundi hilo, Mullah Omar Mullah alifariki mwaka mmoja uliopita katika shambulizi lililofanywa na majeshi ya Marekani.

Maelfu waandamana London kupinga matokeo ya kura ya kujitoa EU
Khloe Kardashian afichua siri ya maisha kati yake na The Game