Kiongozi wa kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria Aboubakar Shekau amejeruhiwa vibaya kwenye shambulio la anga lililofanywa na jeshi la nchi hiyo, taarifa ya jeshi hilo imesema kuwa makamanda wengine wakuu wa kundi hilo pia wameuawa katika shambulio hilo.

Aidha  jeshi la anga la Nigeria limesema shambulio hilo lilifanyika  Ijumaa tarehe 19 Agosti wakati viongozi hao walipokuwa wakishiriki sala ya Ijumaa katika kijiji cha Taye, eneo la Gombale katika msitu wa Sambisa jimbo la Borno.

Kwa mujibu wa jeshi hilo  makamanda  waliouawa ni pamoja na Abubakar Mubi, Malam Nuhu, na maalam Hamman.

 

Viongozi wa CUF wagoma kumpa mkono Profesa Lipumba
Wananchi Wanaoishi Karibu Na Migodi Walalamika Kulipwa Fidia Kidogo