Operesheni ya Jeshi la Marekani iliyoendeshwa nchini Somalia, imesababisha mauaji ya watu 10 akiwemo Afisa kiongozi wa kundi la Islamic State, Bilal al-Sudani katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa ya Jeshi hilo, iliyotolewa kwa vyombo vya Habari imeeleza kuwa Bilal, aliyetajwa na Marekani kama kiongozi wa ISIS nchini Somalia, aliuawa katika operesheni pamoja na watu hao 10 ambao ni washirika wa ISIS.

Wanajeshi wa Marekani wakiwa na kikosi cha Somalia huko Danab. Picha ya US Air Force.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa, operesheni hiyo iliidhinishwa na Rais Joe Biden mapema wiki hii, na kuendeshwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Hata hivyo, Marekani walikataa kujadili maelezo ya msingi kuhusu operesheni hiyo wala kueleza tishio lolote la moja kwa moja lililosababishwa na Sudani kwa Marekani, ikiwa taarifa zozote za kijasusi zilikusanywa, jinsi jeshi la Marekani lilivyoendesha operesheni hiyo na ni wanajeshi wangapi walihusika katika operesheni hiyo.

Wananchi waomba usalama kwa Rais
Museveni aadhimisha miaka 37 madarakani