Kiongozi wa chama cha upinzani (The Left Party Parliamentary) nchini Ujerumani, Sahra Wagenknecht amekumbwa na tukio la aina yake katika kikao cha ndani cha chama hicho baada ya kutoa matamshi yanayopinga wahamiaji na wakimbizi kuingia nchini humo.

Wajumbe wa mkutano huo ambao walionesha kuchukizwa na kauli ya kiongozi huyo walitumia vyakula vilivyotengenzwa kwa chocolate kumpaka uso mzima kuonesha hasira zao.

Picha zilizonaswa na paparazzi dakika chache baada ya kufanyiwa ‘timbwili’ hilo zilimuonesha akiwa amevurugika sura iliyotapakaa misosi kabla ya kusaidiwa kujinusuru na aibu hiyo.

Mama huyo alikumbwa na mkasa huo baada ya kutamka kuwa “sio kila mkimbizi anaweza kwenda Ujerumani.”

Nchi hiyo imekuwa katika wakati wa mvutano kuhusu idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji wanaokimbia hali za hatari katika nchi zao wanawasili tutafuta maisha salama. Baadhi ya wananchi wanaona kundi hilo kama tishio kwa ajira zao na rasilimali.

Serikali yapiga marufuku ‘pombe za viroba’
Chris Brown amchapa Shavu Wizkid

Comments

comments