Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change, Morgan Tsvangirai amemteua mmoja kati ya makamu wake kuwa rais wa chama hicho katika kipindi ambacho anaendelea kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani nchini Afrika Kusini.

Luke Tamborinyoka, msemaji wa Tsvangirai amesema kuwa kiongozi huyo amemteua Nelson Chamisa kukaimu nafasi yake hadi afya yake itakapoimarika na kurejea.

Nelson Chamisa

“Uamuzi huu unatokana na rais wa chama chetu kutokuwepo ofisini kwa sasa na pia kuna makamu wake wawili ambao wote wako Afrika Kusini,” alisema Tamborinyoka.

Kumekuwa na hofu kuwa huenda chama hicho kikuu cha upinzani kikaingia katika mgogoro wa madaraka kuelekea katika uchaguzi mkuu wa nchi.

Rais Emmerson Mnangagwa ameahidi kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki.

Mlinga amfumua Ndalichako kuhusu Shule za serikali kushika mkia
Mashua mbili zazama na kuua watu