Kiongozi wa majambazi yaliovamia Benki ya Access tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kuwaua watu sita  na kabla ya kupora kitita cha shilingi milioni 20, anadaiwa kutiwa mbaroni na kikosi maalum cha Jeshi la Polisi kinachowahusisha pia wanajeshi.

Vyanzo vya kuaminika vimeeleza kuwa kiongozi huyo wa majambazi 12 waliotekeleza tukio hilo alikamatwa jana majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Sinza Mori jijini Dar es Salaam, baada ya kutajwa na majambazi wenzake waliokamatwa siku chache zilizopita.

Majambazi hao wanne walikamatwa wakiwa katika msikiti mmoja ambapo mwenzao alikuwa anafunga ndoa.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe jana aliongea na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Saalm, Simon Sirro lakini alisema kuwa alikuwa hajapata taarifa rasmi kuhusu kukamatwa kwa kinara huyo wa ujambazi kutoka kwa wasaidizi wake.

“Sina chochote hadi sasa, ningekuwa nacho kwanini nikunyime wakati ni jambo la sifa kwetu,” Kamanda Sirro anakaririwa na gazeti hilo.

Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch imetangaza kupambana na majambazi nchini ikiwa ni pamoja na kutumia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pale inapobidi, kuhakikisha inawasaka na kuwafyeka mtandao  wa ujambazi.

 

Washindi Tuzo za Oscar: Leonardo abeba ndoo nzito zaidi, Orodha kamili
Mbowe, Ukawa wavuta pumzi ya mwisho uchaguzi Meya Dar, Zanzibar