Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amemuita katika kikosi chake kipa wa maafande wa JKT Ruvu, Said Kipao.

Mkwasa kamjumuisha chipukizi huyo kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi aliyefiwa na baba yake jana hivyo kushindwa kujumuika na kikosi cha Taifa Stars kitakachoondoka nchini kuelekea Nigeria siku ya Jumatano.

Kipao aling’ara kwa kuzuia michomo ya washambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo, Frederic Blagnon na Shiza Kichuya Katika pambano lililomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Amesajiliwa na JKT Ruvu msimu huu kutoka kituo cha kunoa makipa kinachoendeshwa na kipa wa zamani wa Taifa Stars na Yanga, Peter Manyika.

Mchezo Wa Yanga SC Vs Ruvu JKT Waahirishwa
Vijana Chini Ya Umri Wa Miaka 17 Wamkuna Kocha Azam FC