Kipa Saveli Kononov wa timu ya Izhstal Izhevsk, mwenye umri wa miaka (23), nchini Urusi, amepewa zawadi ya silaha aina ya AK-47 baada ya kuibuka mchezaji bora wa mechi, walipocheza dhidi ya Chelmet Chelyabinsk.

Zawadi hiyo alipewa katika vyuma vya kubadilishia nguo kutoka kwa viongozi na nahodha wa timu yake ambapo wamesema kuwa “tunatoa zawadi hii kwa alivyosaidia kupangua mashuti 36 kati ya 38 yaliyolenga goli, ikitokea tumecheza vibaya basi atatushoot nayo”

Mechi hiyo ilichezwa mapema wiki hii huku timu yake ikibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya wapinzani wao.

Ni utamaduni uliozoeleka  kutoa zawadi zisizo za kawaida kwa wachezaji watakao cheza vizuri Katika ligi ya ‘The National Hockey League’.

Zawadi  nyingine iliyowahi kushangaza ni ya mchezaji wa timu ya Carolina Hurricanes, baada ya kutangazwa kuwa ‘Man Of The Match’ alipewa zawadi ya shoka.

Ndayiragije atangaza watakaoivaa Sudan
Siri ya Maziwa kwa wazee na watoto, Kunywa lita 100