Mlinda mlango wa timu ya KMC inayoshiriki ligi Kuu Tanzania Bara, Denis Richard, amesema upweke wa kufanya mazoezi ya kipekee unamfanya atamani ligi irejee ili aweze kujumuika pamoja na wenzake.

Denis kabla ya kutua KMC kwa watoto wa Kinondoni aliwahi kukipiga kwa vinara wa Ligi hiyo Simba na kujikuta akikosa nafasi ya kuonyesha uwezo wake na kulazimika kuangalia maisha mapya.

Akizungumza na Mwanaspoti Denis amesema, kwa sasa yeye anajifua katika fukwe za Escape Jijini Dar es Salaam ili kulinda kiwango chake wakati huu ligi imesimama.

Anasema kipindi hiki ni kugumu kwao wachezaji lakini hawana namna ya kufanya kutokana na hali halisi ndio sababu ya kujituma kwake ili ikirejea asijekuwa na shida.

“Nafanya mazoezi yangu mwenyewe Escape hapo awali nilikuwa nafanyia nyumbani lakini kwa sasa nimehamia ufukweni, tumuombe Mungu maisha yarejee kama kawaida,”

Aidha Denis anabainisha kuwa. Hata wao wachezaji wamemis kucheza na kuonana na mashabiki zao uwanjani hivyo ligi irejee tu watu wajumuike kwa pamoja.

Anasisitiza kwa kuwataka wachezaji wenzake huko majumbani waliko wasibweteke bali watumie muda huo wa kukaa nyumbani kujirinda viwango vyao.

KMC ina makipa watatu Juma Kaseja, Jonathan Nahimana na Denis.

Watoto 'waliofunga ndoa' wazungumza
Afisa aliyetemewa mate na mgonjwa wa corona afariki