”Simba walinifuata, nitafute kadi ya njano, wanipe IST mpya”,  hayo ni maneno ya mlinda mlango wa klabu ya Yanga, Ramadhan Kabwili ambapo amesema kuwa  uongozi wa Klabu ya Simba umewahi kumlaghai ukimtaka atafute kadi ili asiweze kucheza katika mchezo wa watani wa jadi na kimuahidi akifanya hivyo kumpatia garia iana ya IST.

Mlinda mlango huyo amesema hayo wakati akifanya mahojiano na EATV Radio katika kipindi cha Kipenga Extra mapema leo Jumatatu ya tarehe 27, 2020.

“Simba waliwahi kunifuata kipindi tupo na kocha Zahera, nilikuwa na kadi 2 za njano na kwenye mchezo wa Yanga na JKT Tanzania, walitaka nitafute kadi ya njano makusudi ili wanipe gari ya IST mpya na nikose mchezo ujao wa watani” – Ramadhan Kabwili.

Amesema kuwa tukio hilo lilitokea kipindi ambacho Zahera akiwa kocha wa klabu hiyo ya Yanga.

Amesema kuwa siku hiyo Yanga ilikuwa inaelekea kucheza na JKT Tanzania na yeye alikuwa na kadi mbili za njano, hivyo Simba walimfuata na kumuambia kuwa atafute kadi moja ya njano ili akose mchezo uliokuwa unafuatia wa watani wa jadi huku wakimuahidi kumpa IST mpya, wakiamini kuwa angekaa Klaus Kindoki golini wangemfunga kirahisi.

Katika mchezo huo dhidi ya JKT Tanzania, Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 ambapo Ramadhan Kabwili ndiye alikuwa golikipa wa Yanga siku hiyo.

Aidha Kabwili amesema kuwa kwa sasa ahitaji meneja yoyote atakayemtafutia timu ya Tanzania akitamani meneja ambaye atamtafutia timu Ulaya, “mimi nataka meneja ambaye atanipeleka kucheza soka la Ulaya, sitaki meneja wa kunichezesha hapa nchini kwa sababu kama ni hapa nchini sasa hivi nipo katika klabu kubwa Tanzania na inashinda mataji”.

Orodha kamili ya watu 'wanane' waliofariki dunia wakiwa na Kobe Bryant
Video: ACT wazalendo yatangaza mchakato kugombea uongozi ndani ya chama

Comments

comments